Jeneza la bwana Kibaki limefunikwa bendera ya taifa mapema leo likisindikizwa na wanajeshi kuelekea bungeni ambako litalala kuanzia leo hadi Jumatano.
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuuongoza umma katika kutoa heshima na kuutazama mwili wa hayati kibaki.
Bunge la Kenya ambalo kwa sasa liko mapumzikoni litakuwa na kikao maalumu siku ya Jumatano kumuenzi Kibaki.
Wiki iliyopita rais Kenyatta alitangaza kipindi cha maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti hadi hayati Kibaki atakapozikwa. Kibaki atazikwa kitaifa na heshima zote za kijeshi.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kipindi cha maombolezo kitaifa na bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo cha rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki.
“ Kama kiongozi mkuu katika historia ya kenya baada ya uhuru , Mwai Kibaki alipata heshima na mapenzi makubwa ya watu wa taifa hili na mataifa mengine duniani kote.
“Rais Kibaki atakumbukwa daima kama mwanasiasa muungwana wa kenya , mtoa mada mahiri ambaye ufasaha, na haiba yake vilishinda daima,”ameeleza Rais Kenyatta.
Baada ya kuondoka madarakani mwaka 2013 , kibaki alijihusisha kwa mara chache katika maisha ya umma.
Alianza kuugua mwaka 2016 na maafisa wa serikali na familia yake hawakuwa wakitoa taarifa za afya yake.
Alifurahia maisha mazuri ya afya yake wakati mwingi wa maisha ya utu uzima, akijulikana kuwa mcheza golf wa kudumu nchini humo hadi alipojeruhiwa katika ajali ya barabarani mwaka 2002.
Kibaki amelitumikia taifa la Kenya kama rais wa tatu kwa miaka 10 kuanzia mwaka 2002-2013 na kama mbunge kwa miaka 50 mwaka 1963-2013.
Facebook Forum