Msemaji wa serikali anasema kundi dogo la wanamgambo liliingia katika jengo la ofisi ya waziri mkuu jana asubuhi wakidai malipo kwa waliokuwa wapiganaji waliokuwa wakimpinga Gadhafi.
Upinzani huo baade uliongezeka na kufikia watu 200, wakiwemo wanamgambo kutoka maeneo ya milimani ya magharibi mwa nchi, na kiasi cha magari makubwa 50 yaliyokuwa na silaha.
Msemaji anasema baadhi ya waasi waliingia ndani ya jengo na kufyatua risasi kutokea ndani, wakati wengine walikuwa wakifyatua risasi wakiwa kwenye eneo la jengo hilo.
Afisa usalama anasema waandamanaji 14 walikamatwa.
Serikali ya mpito ya Libya imetoa mishahara kwa waliokuwa wanamgambo ambao walipigana katika mapinduzi ya mwaka jana yaliyomng’oa mamlaka kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Moammar Gadhafi.