Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 27, 2023 Local time: 22:21

Wanajihadi 35 wahukumiwa adhabu ya kifo Libya


Wanajihadi waliokuwa wakituhumiwa kuwa wanachama wa kundi la Islamic State (IS) walipokuwa Misrata, kaskazini-magharibi mwa Libya, tarehe 29 Mei 2023. Picha na Mahmud Turkia / AFP.

Mahakama nchini Libya siku ya Jumatatu iliwahukumu adhabu ya kifo wanajihadi 35 waliokutwa na hatia ya kupigana pamoja na kundi la Islamic State katika nchi hiyo iliyopo Afrika kaskazini.

Watuhumiwa waliungana na IS wakati wa machafuko baada ya kuangushwa kwa utawala wa dikteta Moamer Kadhafi, waandishi wa habari wa AFP waliokuwa katika mahakama hiyo walisema.

Hili lilikuwa kundi la kwanza la wanajihadi 320 wanaodaiwa kuhusika na kundi la IS kufikishwa mahakakani na kuhukumiwa.

Mwaka 2015 Kundi la IS liliuteka mji wa kati wa pwani wa Sirte na kuweka ngome kabla ya kuondolewa mwaka unaofuatia na vikosi vinavyoitii serikali ya kitaifa iliyokuwa madarakani wakati huo, ambapo makao yake makuu yake yalikuwa mjini Tripoli.

Washtakiwa wengine 13 walihukumiwa vifungo vya maisha, baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa mwezi Agosti mwaka jana katika mji wa magharibi wa Misrata, waandishi wa habari wa AFP walisema.

Washtakiwa walikuwa Wapalestina, Wasudan na Walibya. Wote walikuwa wamewekwa kizuizini tangu mwezi Desemba mwaka 2016 na kukutwa na hatia ya kujiunga na kundi la kigaidi, pamoja na mauaji.

Baadhi yao waliachiliwa lakini idadi kamili ya walioachiwa haijajulikana.

Aidha, mahakama hiyo iliwahukumu watoto watatu viifungo vya miaka 10 jela kila mmoja, alisema wakili Lotfi Mohaychem, ambaye aliziwakilisha familia dhidi ya wapiganajaji wa kundi la IS, waliouawa katika mapambano ya Sirte.

Washukiwa hao walionekana kizimbani wakiwa wamevalia ovaroli za rangi ya bluu, wakiwa na ndevu na vichwa vyao vikiwa vimenyolewa.

Ndugu wa waliouawa katika mapambano ya Sirte walijaa mahakamani.

Libya ilitumbukia katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja wa machafuko na uvunjifu wa sheria kufuatia uasi wa mwaka 2011 ulioungwa mkono na NATO ambayo yalisababisha kuondolewa madarakani na kuuawa kwa dikteta wa muda mrefu Kadhafi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG