Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 07:42

Wanajeshi wadai kupindua serikali ya Niger


Rais wa Niger Mohamed Bazoum alipokuwa Berlin Ujerumani, Julai 8, 2021. Picha na Bernd von Jutrczenka/Pool kupitia REUTERS.
Rais wa Niger Mohamed Bazoum alipokuwa Berlin Ujerumani, Julai 8, 2021. Picha na Bernd von Jutrczenka/Pool kupitia REUTERS.

Wanajeshi wamedai kuipindua serikali ya Niger siku ya Alhamisi kufuatia mapinduzi ya dhahiri katika nchi hiyo tete baada ya walinzi wa Rais kumzuia Rais Mohamed Bazoum.

Kikosi maalum cha walinzi wa rais waliokasirishwa walifunga njia kuelekea makazi ya rais na maofisi katika mji mkuu wa Niamey siku ya Jumatano na baada ya mazungumzo kuvunjika wakikataa kumwachilia rais huyo chanzo cha rais kilisema.

Sisi vikosi vya ulinzi na usalama tumeamua kuuondoa utawala wa Rais Bazoum, alisema Kanali-Meja Amadou Abdramane katika hotuba yake kwenye televisheni akiwa amezungukwa na wanajeshi wengine tisa waliovalia sare.

Walisema taasisi zote nchini zitasitishwa mipaka itafungwa, na amri ya kutotoka nje imewekwa hadi taarifa zaidi.

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Afrika zote zilishutumu kile walichokiita jaribio la mapinduzi.

Chanzo kilicho karibu na Bazoum kilitumia neno hilohilo, kikisema kwamba mpango huo hautafaulu.

Mkuu wa ECOWAS amesema Rais wa Benin Patrice Talon alikuwa anaelekea Niger katika jitihada za kutafuta upatanishi baada ya msukosuko wa hivi punde kulikumba eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG