Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:28

Wanajeshi wa Ukraine wadhibithi miji kadhaa na kurusha Kombora Russia


Mabaki ya ndege ya helicopter ya Russia katika kijiji cha Malaya Rohan, eneo la Kharkiv, nchini Ukraine, Monday, May 16, 2022. (PICHA: AP Photo/Bernat Armangue)
Mabaki ya ndege ya helicopter ya Russia katika kijiji cha Malaya Rohan, eneo la Kharkiv, nchini Ukraine, Monday, May 16, 2022. (PICHA: AP Photo/Bernat Armangue)

Wanajeshi wa Ukraine wameendelea kupiga hatua kubwa katika kuwafurusha wanajeshi wa Russia katika sehemu zilizo karibu na Kharkiv, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Ukraine imesema kwamba wanajeshi wake wamefika kwenye mpaka na Russia, ulio kilomita 40 kaskazini mwa Kharkiv.

Wanajeshi hao vile vile wamewasukuma nyumba wanajeshi wa Russia hadi karibu na mto Siverskiy Donets, ulio kilomita 40 mashariki mwa nchi hiyo, na huenda wakavuruga mikakati ya kuwafikishia silaha na chakula wanajeshi wa Russia walio Donbas.

Wanajeshi wa Russia hata hivyo wanaendelea kupigana licha ya kupoteza sehemu kadhaa, wakiwa wameshindwa kuvuka mto huo.

Ofisi ya rais wa Ukraine Zelenskiy, imesema kwamba wanajeshi wa Russia walio kwenye msitari wa mbele, karibu na Donetsk, wanashambulia kabisa na wanajeshi wa Ukraine.

Mkuu wa jeshi wa Ukraine amesema kwamba wanajeshi wa Russia wameendelea kujipanga upya na kujitayarisha kwa mashambulizi mapya karibu na Slovyansk na Drobysheve, kusini mashariki mwa mji wa Izium.

Wanajeshi wa Russia wameshambulia sana sehemu zilizo karibu na Kyiv na mji wa magharibi wa Lyiv, karibu na mpaka na Poland.

Milipuko kadhaa imesikika Lyiv mapema jumanne. Kombora moja limepiga kambi ya kijeshi lakini hakuna kifo kimeripotiwa.

Wanajeshi wa Ukraine wameshambulia kijiji kimoja kilicho katika jimbo la Kursk magharibi mwa Russia karibu na Ukraine, jumanne asubuhi.

Nyumba tatu na shule vimeharibiwa katika shambulizi hilo lakini hakuna kifo wala majerihi wameripotiwa.

XS
SM
MD
LG