Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:36

Wanajeshi wa Russia wanashambulia sehemu za mashariki mwa Ukraine huku Marekani ikituma silaha zaidi


Mwanamke akiondoka katika nyumba inayoungua moto baada ya kupigwa bomu na wanajeshi wa Russia katika mji wa Lysytsansk mashariki mwa Ukrain. May 30, 2022
Mwanamke akiondoka katika nyumba inayoungua moto baada ya kupigwa bomu na wanajeshi wa Russia katika mji wa Lysytsansk mashariki mwa Ukrain. May 30, 2022

Wanajeshi wa Russia wameendelea na mapigano mashariki mwa Ukraine, wakiwa na lengo la kudhibithi sehemu hiyo, huku Marekani itatoa msaada wa roketi zenye nguvu zaidi ili kusaidia wanajeshi wa Ukraine, katika hatua ya kulazimisha Russia kukubalikufanya mazungumzo ya kumaliza vita hivyo.

Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema kwamba wanajeshi wa Russia wanaharibu miundo mbinu mashariki na kusini mwa Ukraine.

Vita vya Ukraine vimeingia siku 98.

Wanajeshi wa Russia wanaendelea na mashambulizi ya kuharibu mji wa viwanda wa Sievie-rodo-netsk, ambao waliingia May 27.

Mji wa Sie-viero-do-netsk unatambulika sana tangu utawala wa Kisovieti, na wenye viwanda vikubwa vya kemikali.

Kulingana na gavana wa mji huo, shambulizi la kombora la Russia lilipiga kiwanda kikubwa cha kemikali mjini humo jana jumanne, na kuharibu kabisa tenki la kemikali yenye sumu.

Rais wa Mrekani Joe Biden ametangaza msaada wa roketi za masafa marefu za kukabiliana na makombora ya Russia, pamoja na risasi. Msaada huo ambao ni sehemu ya msaada wa dola milioni 700, unatarajiwa kuwasili Ukraine hii leo.

XS
SM
MD
LG