Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 19:06

Wanajeshi wazidi kuwasili Sudan Kusini


Wanajeshi wa kigeni katika harakati za kulinda amani Sudan Kusini
Wanajeshi wa kigeni katika harakati za kulinda amani Sudan Kusini

Idadi kubwa ya wanajeshi wa nchi za nje wanaendelea kuwasili katika mji mkuu wa Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya kikosi cha ulinzi cha kikanda (RFP) kilichopendekezwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini mchambuzi mmoja wa Sudan Kusini anasema walinda amani wa ziada hawatabadilisha lolote kwenye nchi hiyo yenye mgogoro unaosababisha vifo kama wanajeshi hawatapelekwa nje ya mji wa Juba.

Wanajeshi zaidi kutoka Rwanda waliwasili siku ya Jumamosi kuungana na kiasi cha wanajeshi 600 kutoka Rwanda, Ethiopia, Bangladesh na Pakistan.

Walinda amani wa UNMISS wakiwa Juba, Sudan Kusini
Walinda amani wa UNMISS wakiwa Juba, Sudan Kusini

​Kulingana na mamlaka waliopewa na Baraza la Usalama mwaka 2016 ni kwamba RPF inatoa ulinzi kwa maeneo muhimu na barabara za huko Juba na kuimarisha usalama kwenye maeneo ya raia yanayolindwa na RPF mahala ambapo maelfu ya watu waliokoseshwa makazi Sudan Kusini wamekuwa wakiishi baada ya mapigano kuzuka katika miji na vijiji vyao.

Mchambuzi wa sera Augustino Ting Mayai wa taasisi ya SUDD yenye makao yake Juba anasema mji mkuu upo thabiti hivyo basi hakuna sababu ya wanajeshi wapya kuwasili na kuendelea kukaa mjini Juba.

Mwezi Agosti mkuu wa UNMISS, David Shearer alisema kuwasili pamoja na awamu nyingine ya vikosi vya RPF kutasaidia kuonekana kwa walinda amani wa UNMISS na kuongeza uwepo wao kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mgogoro nje ya Juba.

XS
SM
MD
LG