Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:31

Wanajeshi wa Israel wamemuuwa raia wa Palestina


Wanamgambo wa Israel katika majibizano ya silaha na waandamanaji wa kipalestina
Wanamgambo wa Israel katika majibizano ya silaha na waandamanaji wa kipalestina

Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Nablus ambako wanajeshi wa Israel walikuwa wakiwasindikiza raia wa Israel kwenye kaburi linalogombaniwa

Wanajeshi wa Israel walimuua kwa kumpiga risasi mwanamume mmoja wa Kipalestina Alhamisi huko Ukingo wa Magharibi eneo wanalolikalia kimabavu kwa kile jeshi la Israel lilisema ni mapambano na wanamgambo.

Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Nablus ambako wanajeshi wa Israel walikuwa wakiwasindikiza raia wa Israel kwenye kaburi linalogombaniwa.

Jeshi la Israel limesema wanamgambo wa Kipalestina walirusha vilipuzi na kuwafyatulia risasi wanajeshi wake ambao walijibu kwa risasi.

Maafisa wa afya wa Palestina wamemtaja mtu aliyefariki kuwa ni Ahmed Daraghmeh, mwanasoka kutoka mji ulio karibu. Shirika la habari la Agence France-Presse (AFP) iliripoti kundi la wanamgambo la Hamas limesema alikuwa sehemu ya kitengo cha jeshi lake.

XS
SM
MD
LG