Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 06:24

Wanajeshi nchini Mali wameuawa na wanajihadi


Nchi ya Mali na majirani zake

Mapigano kati ya miji ya Mopti na Segou pia yalisababisha vifo vya wanajihadi saba jeshi limesema katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa kuamkia Jumatano

Wanajeshi watatu waliuawa na watano walijeruhiwa katika mapambano na wanajihadi katikati mwa Mali siku ya Jumanne jeshi limesema.

Mapigano kati ya miji ya Mopti na Segou pia yalisababisha vifo vya wanajihadi saba jeshi limesema katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa kuamkia Jumatano.

Mapigano hayo yalizuka baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya vikosi vya usalama kwa kutumia vifaa vya milipuko vilivyoboreshwa (IEDs) ilisema.

Mali inakabiliwa na mzozo wa kiusalama uliodumu kwa takriban miaka 11 uliosababishwa na uasi wa kikanda katika eneo la kaskazini ambalo liligeuka kuwa uasi mkubwa wa wanajihadi.

Maelfu ya watu wamekufa, maelfu wamekimbia makaazi yao na uharibifu mkubwa wa kiuchumi umetokea katika moja ya nchi maskini zaidi duniani.

Mwaka 2015, uasi huo ulisambaa hadi nchi jirani za Niger na Burkina Faso.

Tangu Agosti 2020 Mali imekuwa ikitawaliwa na jeshi na kusababisha mvutano na Ufaransa mshirika wa jadi wa nchi hiyo na mwenye uhusiano wa karibu na Russia.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jumanne ilisema hali ya usalama "imeendelea kuzorota katika eneo la kati la Sahel hasa katika nchi za Burkina Faso na Mali."

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG