Wiki moja baada ya mvua kubwa kuanza Jeshi la taifa la ulinzi la Afrika Kusini (SANDF) lilisema Jumatatu limeagizwa kupeleka wanajeshi 10,000 kwa ajili ya kazi ikiwa ni pamoja na kusafisha na kusaidia kusafirisha misaada.
Jeshi hilo pia litatoa msaada wa matibabu na helikopta kwa operesheni za uokoaji na ufuatiliaji.
Mafuriko hayo yamewaacha maelfu bila makazi, yameondoa huduma za umeme na maji na kutatiza shughuli katika mojawapo ya bandari zenye shughuli nyingi zaidi barani Afrika, Durban.