Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:34

Wanainchi wa Guinea Bissau wapiga kura kulichagua bunge jiypa


Mpiga kura akipiga kura yake kwenye kituo kimoja nchini Bissau, Juni 4, 2023.
Mpiga kura akipiga kura yake kwenye kituo kimoja nchini Bissau, Juni 4, 2023.

Wananchi wa Guinea Bissau wamepiga kura leo Jumapili katika uchaguzi wa bunge ulioitishwa na rais ambaye anashinikiza mabadiliko ya katiba baada ya miaka kadhaa ya ukosefu wa usalama katika taifa hilo dogo la Afrika magharibi.

Baada ya kutangaza hivi karibuni kwamba kulikuwepo na jaribio la mapinduzi mwezi Februari 2022, Rais Umaro Sissoco Embalo alilivunja bunge la taifa mwezi Mei baada ya kutofautiana na wabunge na kusababisha nchi kukumbwa na msukosuko wa kisiasa.

“Kawaida huwa kunatokea vurugu baada ya kura kuhesabiwa. Lakini wakati huu nina matumaini makubwa kwamba vurugu hazitatokea. Mgombea bora ashinde na amani itawale kote nchini,” Amesema Fode Malam Faty, mwenye umri wa miaka 55, ambaye ni mufuasi wa chama cha Social Renewal (PRS) baada ya kupiga kura yake.

Guinea Bissau, yenye watu milioni 2 , imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa muda mrefu kufuatia mapinduzi ya mara kwa mara tangu ijipatie uhuru kutoka kwa Ureno mwaka wa 1974.

Forum

XS
SM
MD
LG