Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 08:03

Wanainchi wa Chad wapiga kura katika uchaguzi wa rais uliosusiwa na upinzani


Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby akipiga kura yake katika uchaguzi wa rais mjini N'Djamena, Mei 6, 2024. Picha ya Reuters
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby akipiga kura yake katika uchaguzi wa rais mjini N'Djamena, Mei 6, 2024. Picha ya Reuters

Wananchi wa Chad Jumatatu wamepiga kura katika uchaguzi wenye lengo la kumaliza miaka mitatu ya utawala wa kijeshi lakini uliosusiwa na wapinzani wa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby.

Wataamua ikiwa wanataka kuongeza miongo mitatu ya utawala wa familia ya Deby, katika nchi hiyo muhimu katika vita dhidi ya uasi wa wanajihadi katika eneo la jangwa la Sahel.

Mpinzani mkuu kwenye kinyang’anyiro cha rais ni waziri mkuu Succes Masra, anayeshtumiwa na wakosoaji kuwa kibaraka kwa kutokuwepo wapinzani wengine wakubwa.

Wagombea wote wawili wameapa kushinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, ambao mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yanaonya kuwa hautakuwa huru au wa haki

Forum

XS
SM
MD
LG