Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:42

Wanaharakati washambulia uwanja wa ndege wa Mogadishu


Maafisa wa usalama wa Somalia wanasema gari lililoendeshwa na mjitoa mhanga kuripua bomu limeripuka kwenye mlango mkuu wa uwanja wa ndege wa Mogadishu, na kusababisha vifo vya watu wanane.

Maafisa wa usalama wa Somalia wanasema bomu lililotegwa ndani ya gari limeripuka nje ya mlango mkuu wa uwanja wa ndege wa Mogadishu siku ya Alhamisi na kusababisha vifo vya takriban watu wanane.

Mashahidi wanasema mjitoa mhanga wa kuripua bomu aliendesha gari hilo na kuligonga kwenye kituo cha ukaguzi cha kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nje ya uwanja wa ndege. Wanasema, baada ya mripuko huo walisikia mapigano ya bunduki.

Polisi haijaweza kusema idadi ya walojeruhiwa kutokana na shambulio hilo na wala haijulikani ikiwa walinda amani ni miongoni mwa walouwawa au kujeruhiwa katika shambulio.

Kundi la wanaharakati la al-Shabab lilitangaza hivi karibuni kampeni mpya ya kujaribu kuipindua seriklai ya Somalia na kutangaza utawala wa Sharia za kislamu nchini humo. Mwezi uliyopita wanaharakati walishambulia hoteli wanakoishi wabunge wengi na kuwauwa watu 33 wakiwemo wabunge wanne.

Wiki iliyopita, Umoja wa Afrika ulitangaza kwamba unaimani kwamba majeshi ya serikali na walinda amani watawashinda al_Shabab.

XS
SM
MD
LG