Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 12:41

Wanaharakati wa mazingira waandamana kwenye mkutano wa COP27


Jina la COP27 karibu na ukumbi wa mkutano wa kimazingira mjini Sharm el-Sheikh, Misri

Wanaharakati wa mazingira Ijumaa wamekusanyika karibu na ikumbi wa mkutano wa kimataifa wa kimazingira nchini Misri, kulalamikia masuala kadhaa yanayohusu bara la Afrika.

Wakiwa wamebeba mabango yenye maneno ya “ msilete janga la mazingira", msiiharibu Afrika kwa gesi pamoja na “, "kuangamiza nishati ya gesi", wameandamana nje ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira wa COP27 nchini Misri, katika mji wa Sharm al Sheikh.

Waandamanaji hao wanadai kuwa washiriki wa mkutano huo wamekwepa kuzungumzia athari za nishati kutokana na mafuta ghafi. Wameongeza kusema kwamba washiriki walihudhuria kwa hisani ya makampuni makubwa ya nishati.

Wamesema pia kwamba washiriki hao wanaweka maisha ya maelfu ya watu hatarini. Alhamisi Umoja wa Ulaya ulitoa mapendekezo kadhaa kama vile kubuni mfuko wa kuyasaidia mataifa masikini kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na kupunguza uzalishaji wa nishati chafu yenye kuharibu mazingira.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG