Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 20:19

Wanaharakati Kenya wataka watenda ghasia za 2008 kuhukumiwa


Mfuasi wa chama cha Orange Democratic Party ODM akibepa panga mbele ya kizuizi kinachowake moto wakati wa ghasia za 2008 katika kitongoji cha Kibera Nairobi.
Mfuasi wa chama cha Orange Democratic Party ODM akibepa panga mbele ya kizuizi kinachowake moto wakati wa ghasia za 2008 katika kitongoji cha Kibera Nairobi.
Mungano wa vyama vya kutetea haki za kiraia unaojulikana kama Wakenya kwa ajili ya Amani wenye Ukweli na Haki, KPTJ, kimezindua ripoti iliyopewa jina la "Securing Justice."

Ripoti hiyo inatoa wito kwa serikali ya Kenya kuunda mahakama maalum kuwahukumu wale walohusika moja kwa moja katika kushambulia watu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi 2008.

Akizungumza mjini Nairobi wakati wa kuzindua ripoti, mratibu wa KPTJ, Bi, Carole Theuri, alisema kunahaja ya kuundwa mahakama itakayowahukumu wale watu wa kawaida walotenda ghasia za 2008.

Mahojiano na James Gondi - 8:59
please wait

No media source currently available

0:00 0:08:58 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mshauri wa mipango wa muungano huo unaokusanya pamoja mashirika ya kiraia na ya kutetea haki za Binadam James Gondi ameiambia Sauti ya Amerika kwamba,

"Mbali na watu waloshtakiwa kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa ICC, kuna orodha ndefu ya watu walotenda maovu, walichoma moto nyumba za watu, waliwabaka wanawake na kuiba mali ya raia, wanaoishi pamoja na wananchi wengine na wanajulikana."

Anasema inabidi kwa watu hao kufikishwa mahakamani na kueleza walichokitenda na kwanini walifanya hivyo na ikiwa walitumwa na mtu.

Bw. Gondi anasema mbali na mahakama kundi lake linataka kuwepo na utaratibu wa upatanishi na maridhiano ili watu wafahamu sababu za ghasia hizo na kujuwa ukweli wa mambo kabla ya amani ya kweli kuweza kupatikana.
XS
SM
MD
LG