Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:34

Wanahabari wawili wauwawa kwenye mapigano ya Gaza


Wanahabari wa Palestina wakiandamana kulalamikia vifo vya wenzao kwenye vita vya Gaza. Nov. 7, 2023. Picha ya maktaba.
Wanahabari wa Palestina wakiandamana kulalamikia vifo vya wenzao kwenye vita vya Gaza. Nov. 7, 2023. Picha ya maktaba.

Wanahabari wawili, Mustafa Thuria ambaye ni mtaalam wa video kutoka shirika la habari la AFP, na Hamza Wael Dahdouh, kutoka Al Jazeera Jumapili wameripotiwa kuuwawa huko Gaza kwenye mashambulizi ya anga ya Israel, wakati taifa hilo likiendelea na operesheni zake za kijeshi dhidi ya kundi la Hamas.

Wawili hao waliuwawa wakati wakiwa kwenye gari lao, kulingana na ripoti kutoka wizara ya afya ya Gaza. Baba ya Hamza ndiye mkuu wa ofisi ya Al Jazeera huko Gaza, na hivi karibuni alijeruhiwa kwenye shambilizi pia, wakati mke wake na watoto wawili wakiuliwa awali, siku chache baada ya vita hivyo kuanza.

Ripoti zaidi zinasema kwamba mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis umeshambuliwa kwenye mashambulizi ya anga Jumapili, ambapo watu kadhaa wamekufa huku wengine wakijeruhiwa.

“Vikosi vya Israel vimesambaratisha mtandao wa kijeshi wa Hamas kaskazini mwa Gaza, wakati wanamgambo 8,000 wakiuliwa, maelfu ya silaha kunaswa, pamoja na mamilioni ya nyaraka kupatikana,” amesema msemaji wa jeshi la Isreal jana Jumamosi.

Forum

XS
SM
MD
LG