Mamia ya vijana wa Kyrgyz walivamia makazi ya wanafunzi katika mji mkuu Bishkek mapema Ijumaa na kuwashambulia wanafunzi wa kigeni.
Polisi, ingawa walikuwapo, hawakuweza kuzuia vurugu hizo.
Serikali ya Pakistani imepanga safari za ndege za ziada kuondoka kila siku kutoka Bishkek na wanafunzi wengi wanatumia fursa hiyo kurejea nyumbani, angalau kwa muda.
Serikali ya Kyrgyzstan imejaribu kuwaondoa hofu wanafunzi wa kigeni na kufanya mikutano na viongozi wao, alisema Yousaf, ambaye alionyesha matumaini kwamba wale wanaoondoka watarejea baada ya miezi michache.
Polisi inawashikilia watu zaidi ya kumi wanaoshukiwa kuhusika na mashambulizi.
Forum