Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:29

Wanafunzi waandamana Washington DC


Karibu wanafunzi 1,000 wa shule za sekondari kutoka Washington DC, na maeneo ya jirani walitoka mashuleni na kuandamana kuzunguka mji hapo Jumanne, wakimpinga rais mteule w Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa mwanafunzi mmoja aliyeongea na VOA alisema kwamba klabu ya haki za binadamu katika shule ya Wilson iliyopo Washington,ilipanga maandamano hayo.

Amesema klabu hiyo iliwafahamisha wanafunzi kupitia mitandao ya kijamii na kuwaandikia wazazi kupitia barua pepe nia yao ya kupanga kutoka mashuleni na kuandamana katikati ya mji hapo jana.

Licha ya kwamba mamia ya wanafunzi hao hawakupiga kura, walitaka kutoa maoni yao kuhusu rais mteule na wasiwasi wao kuhusu mustakabali wao wa baadaye.

XS
SM
MD
LG