Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 13:20

Wanafunzi 15 watekwa nyara Nigeria


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan

Polisi wa Nigeria wanawatafuta watoto 15 wa shule ambao wametekwa nyara

Polisi wa Nigeria wanawatafuta watoto 15 wa shule ambao walitekwa nyara kusini mashariki mwa Nigeria na watu wenye silaha.

Msemaji wa Polisi alisema Jumanne kuwa wateka nyara hao wamedai fidia kutoka kwa wamiliki wa shule binafsi wanayosoma watoto hao.

Waliteka watoto hao baada ya kuteka basi lao jumatatu mapema asubuhi.

Polisi walisema watoto hao walikuwa wanasoma katika shule ya chekechea na shule ya msingi ya Abayi International katika jimbo la Abia.

Kumekuwa na vitendo kadhaa vya utekaji nyara katika jimbo la Abia karibu na eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.

XS
SM
MD
LG