Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 21, 2025 Local time: 18:04

Wamarekani wanufaika na sera za "Bidenomics"-White House


Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba ya sera ya uchumi huko Chicago, terehe 28 Juni 2023. Picha na REUTERS/Leah Millis.
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba ya sera ya uchumi huko Chicago, terehe 28 Juni 2023. Picha na REUTERS/Leah Millis.

Wakati rais Joe Biden anaelekea katika kampeni za kugombea tena urais mwaka 2024, White House limetunga neno la "Bidenomics" ili kutoa hoja kwamba sera za Biden za "kukuza uchumi kutoka chini kwenda juu na kwa mapana na marefu" zimefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza ukosefu wa ajira.

"Sehemu ya Wamarekani wenye umri wa kufanya kazi katika nguvu kazi ni kubwa sasa kuliko ilivyokuwa katika kipindi cha miaka 15," Lael Brainard, mkurugenzi wa Baraza la Kitaifa la Uchumi la White House, alisema Jumanne wakati wa mkutano wa habari. "Wakati tukiwa bado tuna kazi kubwa ya kufanya, mfumuko wa bei umekuwa ukishuka kwa miezi 11 mfululizo."

Alitaja ajira milioni 13 zilizoundwa tangu Biden aingie madarakani mwezi Februari 2021 na kiwango cha ukosefu wa ajira kimesalia chini ya asilimia nne tangu Februari mwaka huu.

Viashiria vya hivi karibuni vya kiuchumi vinaupa utawala sababu za kuwa na matumaini. Ingawa mfumuko wa bei bado unaleta changamoto, waajiri wanaendelea kuajiri, na bei za bidhaa za watumiaji zimekuwa zikipanda kwa kasi ndogo mwezi wa Mei ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Lakini hadi sasa Wamarekani wengi hawakubaliani na matumaini ya utawala ulionayo. Kura za maonio za hivi karibuni zilizipigwa na Ipsos zinaonyesha Biden bado anakubalika kwa asilimia takriban 40.

Uchumi unasalia kuwa suala linalipewa kipaumbele, na wengi wana wasiwasi kuhusu mwelekeo wa nchi, ukweli ni kwamba Warepublican wana hamu ya kutia dosari.

"Inashangaza kwangu kwamba rais anaendelea kuwa na ujasiri wa kusema mambo kama 'familia zinazofanya kazi kwa bidii na zinanufaika na matunda ya sera zake," Kinara wa chama cha Republican katika Seneti John Thune alisema mapema mwezi huu. "Hakika familia zinazofanya kazi kwa bidii zinanufaika na sera za rais, lakini sio thawabu."

Forum

XS
SM
MD
LG