Ni asilimia 10 pekee wanasema demokrasia inafanya kazi vizuri sana, wakati asilimia 40 wanasema kwamba inafanya kazi kiasi. Vyama vikuu viwili vya siasa nchini Marekani- vyote vilipata alama za chini kwa namna vinavyoendesha misingi ya demokrasia.
Asilimia 47 ya watu waliohojiwa walisema kwamba wademokrat wanafanya kazi isiyoridhisha katika kudumisha demokrsia, wakati asilimia 56 wakisema kwamba warepablikan wanahitaji kufanya vizuri zaidi.
Shirika la AP linasema kwamba ukusanyaji maoni unaonyesha kuna migawanyiko mikubwa ya kisiasa, wakati taifa likijikwamua kutokana na janga la corona pamoja na mfumuko wa bei na hofu ya kudorora kwa uchumi. Takwimu hizo zilikusanywa kati ya Juni 22 na 26 mwaka huu.
Forum