Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:53

Wamarekani watiwa khofu na kimbunga Sandy


Huduma za usafiri wa umma huko New York City zimesimamishwa kwasababu ya kimbunga Sandy.
Huduma za usafiri wa umma huko New York City zimesimamishwa kwasababu ya kimbunga Sandy.
Kimbunga Sandy kimeimarika wakati kikiwa kinakaribia eneo la pwani ya mashariki mwa Marekani, na kuwafanya takriban watu milioni 50 kukumbwa na mvua nyingi na upepo mkali kutokana na moja ya dhoruba kubwa kuwahi kulipiga eneo hilo kwa miaka kadhaa.

Miji mikubwa ya Marekani kuanzia Washington mpaka New York ilisimamisha shughuli zake Jumatatu, huku huduma za usafiri wa umma zikisimamishwa, viwanja vya ndege vimefungwa na mamilioni ya watu wamelazimika kutokwenda kazini. Kasi ya upepo kwa kimbunga Sandy ni kilometa 150 kwa saa wakati kilipoanza upande wa magharibi na kuelekea eneo la pwani ya Altantic hapa Marekani.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho kipo kiasi cha kilometa 65 kusini mwa Altantic City huko New Jersey, kiasi cha kilometa 200 kusini mwa New York City na kinasafiri upande wa magharibi kwa kasi ya kilometa 44 kwa saa.

Rais Barack Obama amefuta matukio ya kampeni za uchaguzi kufuatilia dhoruba hiyo kutokea White House. Amewasihi wale ambao wako katika maeneo ambayo kimbunga kinapita kuheshimu maonyo kuhusu hatari za dhoruba hiyo.
XS
SM
MD
LG