Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 14:53

Watu 3 wafariki katika mafuriko Louisiana, Marekani

Mvua nyingi zimesababisha vifo vya takriban watu watatu na mtu mmoja hajulikani alipo kufikia jana.
Mvua nyingi zimesababisha vifo vya takriban watu watatu na mtu mmoja hajulikani alipo kufikia jana.

Gavana wa jimbo la Louisiana lililo kusini mwa Marekani ana ambalo limekumbwa na mafuriko, alionya siku ya Jumapili kwamba kiwango cha maji kinaendelea kuongezeka, huku waokoaji wakiongeza juhudi zao za kujaribu kuwaokoa maelfu ya watu.

Gavana John Bel Edwards alisema wtu wapatao 7,000, wengi wao wakiwa katika eneo la Kusini Mashariki mwa jimbo hilo, tayari wameokolewa kutoka manyumbani na magarini mwao, huku timu za askari wa ulinzi wa kitaifa waliotumia helikopta, pamoja na raia, wakishirikiana kujaribu kupunguza athari za mafuriko hayo.

Mtu avuka barabara iliyofurika maji mjini Hammond, Louisiana.
Mtu avuka barabara iliyofurika maji mjini Hammond, Louisiana.

Mvua nyingi zimesababisha vifo vya takriban watu watatu na mtu mmoja hajulikani alipo kufikia jana.

Kulingana na idara ya kitaifa ya utabiri wa hali ya hewa, zaidi ya sentimita mvua zaidi ya sentimita 50 imenyesha katika sehemu za Louisiana mnamo wiki iliyopita

XS
SM
MD
LG