Makundi ya akina mama hasa maeneo ya Afrika Mashariki na kati yamesaidia kuunganisha wanawake wengi na pia kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mfano ni nchini Kenya ambapo wanawake wengi wamefaidika kutokana na juhudi zao za kuunda makundi ya kibiashara.
Licha ya changamoto zinazowakabili ikiwemo mila na tamaduni, uchumi pamoja na miundo mbinu duni, makundi ya akina mama nchini humo yamejitolea na kupiga hatua kubwa katika shughuli za biashara na maendeleo.
Mwanahabari wetu wa Mombasa alipata fursa ya kutembelea kundi moja la akina mama mjini humo la Sahara Clean Energy linalojishugulisha na utengezaji na uuzaji wa mkaa ya kisasa.
Facebook Forum