Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 18, 2025 Local time: 03:43

Walinda amani wauwawa Mali


Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umesema kuwa walinda amani ishirini wa Umoja huo wamejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa Jumatano katikati mwa Mali wakati wakiwa kwenye kambi yao.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, muungano wa walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Mali, MINUSMA, umesema kuwa kambi hiyo ilioko karibu na mji wa Douentza ilishambuliwa mwendo wa saa moja bila kusema ni nani anaeshukiwa kutekeleza.

Mara nyingi mashambulizi dhidi ya walinda amani pamoja na jeshi la Mali hufanywa na makundi yenye uhusiano na al Qaida na Islamic State ambayo hutumia eneo hilo kufanya mashambulizi kwenye eneo la Sahel, lililoko kusini mwa jangwa la sahara.

Mkuu wa MINUSMA Mahamat Saleh Annadif amesema kuwa wamekuwa wakifanya operesheni za kiusalama kwenye eneo hilo kwa miezi kadhaa sasa.

Amaongeza kusema kuwa operesheni zao zinatatiza adui lakini wataendelea kuzingatia amani ya watu wa Mali. MINUSMA ina zaidi ya wanajeshi 13,000 wanaodhibiti makundi ya wanamgambo katikati na kaskazini mwa Mali.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG