Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:53

Walimu Rwanda wasema  hatua imepigwa kuhakikisha haki na mahitaji yao yanaboreshwa


.Mwalimu akifundisha darasani nchini Rwanda walimu hao wameendelea kufurahia shughuli kubwa iliyofanywa na serikali kuboresha maisha pamoja na kazi yao. (Karemera).
.Mwalimu akifundisha darasani nchini Rwanda walimu hao wameendelea kufurahia shughuli kubwa iliyofanywa na serikali kuboresha maisha pamoja na kazi yao. (Karemera).

Wakati dunia Ikiadhimisha sikukuu ya walimu nchini Rwanda walimu wanasema  kuna hatua iliyopigwa kuhakikisha haki na mahitaji yao vinaboreshwa

Sikukuu hii imeadhimishwa wakati walimu wakiendelea kufurahia shughuli kubwa iliyofanywa na serikali ya Rwanda kuboresha maisha yao.

Ni mwezi uliopita tu ambapo serikali ya Rwanda ilitangaza nyongeza ya mishahara ya walimu kwa kiwango cha asilimia 85%. Sasa wakati walimu wakiadhimisha siku hii, mafanikio haya hawakosi kuyataja.

Licha ya nyongeza hii ya mishahara serikali kwa miaka mingi sasa imekuwa ikiongeza kiasi cha mabilioni ya faranga kwenye chama cha kuweka na kukopa maarufu kama mwalimu SACCOS nchini Rwanda.

Kutokana na mafanikio haya baadhi ya walimu wanasema sasa macho yataelekezwa katika matumizi ya sayansi ya teknolojia hasa kwenye suala la ufundishaji.

Mkuu wa chuo kikuu huria cha Kigali Dk.Rusibana Claude amesema kwamba kuboresha maisha ya mwalimu kuna athari chanya kwa sababu kunainua pia kiwango cha elimu inayotolewa kwa sababu sasa mwalimu anafanya kazi kwa kuridhika na maisha anasema "Jambo la kwanza mwalimu ni mtu ambaye ndiye chimbuko la maarifa na ujuzi tunaouna duniani kila mtu mwenye kufanya jambo la maana amepitia kwenye mikono ya mwalimu sasa unaboresha maisha ya mtu kama huyu maana yake si kwamba unampa hadhi tu lakini unainua kiwango cha kile anachokitoa kwa jamii".

Kwa upande mwingine wiki iliyopita serikali ya Rwanda ilitoa amri ya kuweka viwango sawa vya ada ya shule kwa shule zote za serikali kuanzia msingi hadi sekondari, suala hili liliwafurahisha pia wazazi.

Hata hivyo siku hii pia inaadhimishwa kukiwa bado na baadhi ya changamoto kubwa ikiwa ni suala la idadi kubwa ya wanafunzi kwa baadhi ya shule.

XS
SM
MD
LG