Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 09:40

Wakristo waadhimisha Ijumaa Kuu duniani

Sanamu la Yesu Kristo likionyesha historia ya siku ya Ijumaa Kuu (AP Photo/Moises Castillo).
Sanamu la Yesu Kristo likionyesha historia ya siku ya Ijumaa Kuu (AP Photo/Moises Castillo).

Mjini Jerusalem, maelfu ya waaumini wamejitokeza katika mji huo mtakatifu, baada ya miaka miwili ya utekelezaji wa amri za kupambana na virusi vya Corona.

Wakristo kote duniani wanaadhimisha ijumaa kuu, siku ambayo wakristo wanaamini kwamba Yesu kristo alisulubiwa.

Mjini Jerusalem, maelfu ya waaumini wamejitokeza katika mji huo mtakatifu, baada ya miaka miwili ya utekelezaji wa amri za kupambana na virusi vya Corona.

Waumini kutoka sehemu mbalimbali duniani wamepita kwenye barabara inayoaminikwa kuwa Yesu Kristo alipita akiwa amebeba msalaba, kabla ya kusulubiwa.

Makanisa kadhaa yamefunguliwa kwa waumini kuingia na kufanya ibada.

Baadhi ya waumini wamebeba misalaba iliyotengenezwa kwa mbao, na kuimba nyimbo za kuadhimisha mojawapo ya siku muhimu na takatifu kwa wakristo.

Walisimama katika sehemu tofauti, namna ilivyokuwa wakati Yesu alipokuwa anateswa kabla ya kusulubiwa.

Wakiristo wanaamini kwamba Yesu alifufuka jumapili. Kilele cha maadhimisho itakuwa Jumatatu.

XS
SM
MD
LG