Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 22:19

Wakili wa haki za binadamu Uganda ashitakiwa


Stella Nyanzi akiwa amebebwa na wakili wake Nicholas Opio baada ya kupata dhamana huko Kampala Uganda, May 10, 2017. (Photo: H. Athumani/VOA)

Mahakama moja ya Uganda imemshtaki wakili wa haki za binadamu nchini humo Nicholas Opio kwa biashara haramu ya mzunguko wa fedha kufuatia kukamatwa kwake siku ya Jumanne. Mawakili wa Opio wanasema mashtaka hayo yana ushawishi wa kisiasa kwa sababu ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani na mgombea urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine.

Serikali inadai kwamba mnamo Oktoba 8, katika tawi la Benki ya Absa mjini Kampala, Nicholas Opio alipata $ 340,000 kwa jina la shirika la haki za binadamu Chapter 4. Waendesha mashtaka wanasema wakati huo, alijua pesa hizo zilikuwa za mapato ya uhalifu.

Solomon Muyita ni msemaji wa mahakama anasema

“Mahakama hiyo haina mamlaka ya kushughulikia suala hilo. Kwa hivyo, hakimu alimsomea tu mashtaka na kumpeleka katika gereza la Kitalya hadi Jumatatu wiki ijayo. Faili lake litahamishiwa kwenye mahakama ya kupambana na ufisadi. Na huko ndio litakaposhughulikiwa kwenda mbele. "

Wenzake Opio wawili ambao walikamatwa pamoja naye, wameachiliwa kwa dhamana.

Wakili wa Opio, Eron Kiiza, anasema serikali ilihitaji tu shtaka la kumshikilia Opio, lakini hili halihusiani na kazi yake.

“Wanamsumbua kwa sababu ya kumuunga mkono Bobi Wine. Sio biasahra haramu ya mzunguko wa fedha; wanajua vitabu vyake. Walipekua nyumba yake na hawakupata chochote. ”aliongeza Kiiza.

Wanaharakati wanasema serikali inaharibu kazi za asasi za kiraia na inazitesa asasi hizo za kiraia na viongozi mmoja mmoja.

Msemaji wa polisi wa Uganda Fred Enanga anasema madai hayo hayana msingi wowote na wanapaswa kuruhusu uchunguzi kuthibitisha kutokuwa na hatia au kama anayo hatia.

“Hakuna mwanaharakati ambaye yuko juu ya sheria. Ikiwa wanahusika katika shughuli za kutiliwa shaka, lazima tuwachunguze ili kusaidia kuthibitisha au kutothibitisha baadhi ya madai haya. "alisema Enanga.

Opio, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya haki za binadamu Chapter 4 ya Uganda, alikamatwa na askari kanzu kwenye mgahawa siku ya Jumanne jioni.

Kulingana na Chapter 4, wakati wa kukamatwa kwake, Opio alikuwa akifanya kazi ya kukusanya ushahidi unaohusu mauaji na ukamataji ambao ulitokea baada ya maandamano ya Novemba 18 na 19.

Maandamano hayo yalisababisha kukamatwa kwa Wine, na kupelekea mapambano kati ya vikosi vya usalamana wafuasi wa upinzani. Watu 56 waliuawa.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG