Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:25

Wito watolewa kuwasaidia wakimbizi kusini Mashariki mwa Asia

Makundi ya kutetea Haki za Binadamu yanatoa wito kwa Jumuia ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) kuchukua juhudi zaidi katika kuwapatia makazi kiasi cha wakimbizi 7,000 waislam wa Myanmar, mwaka mmoja baada ya wakimbizi hao kuokolewa baada ya kuachwa baharini na wasafirishaji biashara haramu.

Wakimbizi hao wengi wao wakazi wa Kirohingya, kutoka jimbo la magharibi la Myanmar la Arakine, na waliokolewa baada ya msako uliofanywa na Maafisa wa Thailand.

Awali, makambi yaliyotumiwa na wasafirishaji biashara haramu yaligundulika huko kusini mwa Thailand na darzeni ya miili ilipatikana katika makaburi ambayo hayakuchimbwa sana.

Zaidi ya watu 100 walokamatwa wakihusishwa na magenge ya usafirishaji haramu wa watu, wakiwemo baadhi ya maafisa wa Thailand.

XS
SM
MD
LG