Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 19:52
VOA Direct Packages

Wakimbizi wa Ukraine na Syria wajipata tena kwenye janga la tetemeko la ardhi la Uturuki


Mabaki ya jengo lililoporomoka kutokana na tetemeko la ardhi la Uturuki.
Mabaki ya jengo lililoporomoka kutokana na tetemeko la ardhi la Uturuki.

Wakati vita vilipozuka nchini Ukraine, jamaa wa Aydin Sisman walikimbilia katika mji wa kizamani wa Antakya, eneo la kusini mashariki mwa Uturuki ambalo linapakana na Syria.

Huenda waliepuka janga moja, lakini jingine limewakuta katika makazi yao mapya. Siku ya Jumatatu wiki iliyopita tetemeko kubwa la ardhi la 7.8 kwa kipimo cha rikta lilipiga eneo la Antakya na kuuharibu mkoa huo katika kile ambacho Uturuki imesema ni janga la karne.

Sisman ambaye baba mkwe wake alikwama kwenye kifusi cha jengo la ghorofa kumi alionekana kupoteza matumaini, wakati mamilioni ya wakimbizi kama yeye walikwenda Uturuki kwa ajili ya kujihifadhi dhidi ya vita nchini Ukraine.

Nchini Uturuki pia kuna takriban raia milioni 3. Wa Syria ambao walikimbia mapigano nchini kwao tangu mwaka 2011, waliwasili kwa idadi kubwa, wakipitia mipakani, kutafuta hifadhi salama kuepuka mashambulizi ya mabomu, mashambulizi ya kemikali, na njaa.

Zaidi ya watu wengine 300,000 wamekimbia mizozo na hali ngumu ya maisha kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG