Ujumbe wa maafisa 17 kutoka kundi la kijeshi linalotawala Myanmar umetembelea Bangladesh wiki hii ili kufanya mahojiano na baadhi ya wakimbizi, ambao huenda wakarejea, ikiwa miaka 5 baada ya kufanyika msako mkali wa kijeshi uliopelekea idadi kubwa ya kabila la Rohingya kutoroka makwao.
Ziara hiyo iliyoongozwa na China na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa inaashiria kuanza kwa makubaliano kati ya Maynmar na Bangladesh, ya kuwerejesha wakimbizi baada ya muda mrefu wa wasiwasi kwamba wangeteseka iwapo wangerejea makwao.
Hata hivyo baadhi ya wa Rohingya waliohojiwa na wajumbe hao wameambia shirika la habari la AFP kwamba hawakupata majibu ya kuridhisha kuhusu haki zao za uraia wa Myanmar.