Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:10

Wakimbizi wa Kenya wangali kambini


Kundi moja la wanawake wamebeba kuni za kuwashia moto kwenye kambi ya wakimbizi huko Naivasha Kenya.

Maelfu ya wakenya waliotoroshwa manyumbani mwao wangali wanaishi maisha ya taabu kwenye kambi.

Huku taifa la Kenya likijiandaa kwa uchaguzi mkuu pengine baadaye mwaka huu, na kesi za uhalifu dhidi ya wakenya wanne mashuhuri kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC juu ya kuhusika kwao na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita, maelfu ya wakenya waliotoroshwa manyumbani mwao wangali wanaishi maisha ya taabu kwenye kambi. Wakiungwa mkono na makundi ya kutetea haki za binadamu, wakenya hao waliofukuzwa makwao wametoa mwito kwa serikali ama kuwatafutia makazi bora zaidi ya kuishi au kuwalipa fidia kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Wengi wao wanaishi katika eneo la Maai Mahiu tangu mapema mwaka wa 2008 baada ya kukimbia ghasia za baada ya uchaguzi. Ghasia za kikabila zilizuka Kenya mwishoni mwa mwaka wa 2007 na mwanzo wa mwaka wa 2008 kufuatia mvutano mkali juu ya matokeo ya uchaguzi wa urais. Zaidi ya watu elfu moja waliuawa. Inakisiwa kuwa waliotoroka manyumbani mwao ni kati ya takriban laki 3 hadi laki sita na nusu kwa mujibu wa tume ya haki za binadamu ya Kenya. Mbunge wa eneo la Naivasha John Mututho amewashtaki mahakamani viongozi wa vyama na baadhi ya mawaziri kwa kushindwa kuwasaidia wakimbizi hao. Pia ametoa mwito kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka isiweke mipaka mipya ya maeneo ya uwakilishi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao hadi wakimbizi hao wa ndani wapatiwe makazi bora ya kuishi.

XS
SM
MD
LG