Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 11:30

Wakimmbizi wa DRC waliopo Rwanda wanadai kushambuliwa


Wakimbizi wa DRC
Wakimbizi wa DRC

Wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC waliopo nchini Rwanda walisema wanajeshi wa nchi hiyo waliwafyatulia risasi na kuwajeruhi angalau watu wawili siku ya Jumanne wakati wakimbizi hao wakijaribu kuandamana kutoka nje ya kambi yao wakipinga kupunguzwa kwa mgao wa chakula.

Kulingana na shirika la habari la Reuters waziri mmoja wa serikali alikanusha madai ya wakimbizi hao na alisema watu wapatao 2,000 kutoka kambi ya Karongi yenye wakimbizi 17,000 huko magharibi mwa Rwanda waliandamana na kutoka nje ya kambi wakipinga kupunguzwa kwa asilimia 25 ya posho inayotolewa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa- UNHCR kuanzia mwezi uliopita. Shirika hilo lilipunguza mgao likisema kwamba linakabiliwa na matatizo ya fedha za msaada.

XS
SM
MD
LG