Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:44

Sweden yaweka sheria ya kudhibiti mipaka yake


Sweden yabadili sera yake ya muda mrefu na kuweka udhibiti wa mipaka ili kuzuia mmiminiko wa wakimbizi wanaoingia nchini humo.

Sweden inasema inajiandaa kuondoa kiasi cha watu 80,000 wanaoomba hifadhi ambao wameingia nchini humo kwa idadi kubwa mwaka jana.

Idadi hiyo inawakilisha nusu ya watu 163,000 waliovuka na kuingia Sweden wakikimbia vita nchini Syria, Iraq na Afghanistan. Waziri wa mambo ya ndani Anders Ygeman aliliambia gazeti la Sweden alhamisi kwamba wakimbizi hao watafukuzwa nchini humo kwa sababu maombi yao ya hifadhi yamekataliwa.
Sweden ilikuwa kituo cha juu kwa wakimbizi kwasababu ya sera ya muda mrefu kuhusu mipaka kuwa wazi, lakini idadi kubwa ya wakimbizi hao imeilazimu Stockholm kuweka udhibiti mipakani kwa wakimbizi wapya.

XS
SM
MD
LG