Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:39

Wakenya wasaidia wathiriwa wa janga la njaa


Wakimbizi wa kisomali walowasili wanapokea msaada wa chakula katika kituo cha kugawa chakula cha WFP katika kambi ya Dadaab.
Wakimbizi wa kisomali walowasili wanapokea msaada wa chakula katika kituo cha kugawa chakula cha WFP katika kambi ya Dadaab.

Wananchi wa Kenya wamenaza kampeni ya kuwasiadia raia wenzao wanaokumbwa na janga la njaa kwa kuchangisha fedha na misaada ya dharura.

Kutokana na baa la ukame na vita vinavyosababisha mamilioni ya wakazi wa Somalia na wale wa kaskazini ya Kenya kukabiliwa na njaa, wananchi wa kawaida pamoja na makampuni na mashirika yasiyo ya kiserikali wameanza kampeni kubwa ya kuchanga fedha kuwasaidia wahanga wa janga hilo.

Fedha hizo zinazokusanywa katika kampeni ya kitaifa zinatumiwa kununua chakula, madawa na mahitaji mengine ya kibinadamu kuwasaidia hasa watoto wa kina mama huko kaskazini mashariki ya Kenya.

Katika muda wa siku mbili mfululizo wananchi wamefanikiwa kuchanga zaidi ya dola elfu sabini za kimarekani ili kuwasaidia wahanga wa njaa. Michango hii ni tofauti na msaada unayotolewa na serikali kwa wananchi hao.

Wakati huoi huo maafisa wakuuy wa serikali wanazuru maeno yaliyoathirika na ukame na mjadala umeanza juu ya hatua za kuchukuliwa kukabiliana na janga hilo na namna ya kuzia lisitoke tena.

Viongozi wa kisiasa na wananchi wamekuwa wakiilaumu serikali kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.Lakini Makmu rais Bw. Kalonzo Musyoka anataka watu kuacha kulaumiana, "huu si wakati wa kulaumiana huu ni wakati wa kuokoa maisha ya watu wetu,. Nimeona watu wakilaumiana wengine wanailaumu serikali wakati serikali imetoa 300 milion shillings kwa mwaka huu wa fedha."

XS
SM
MD
LG