Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 11:02

Wakenya wafuatilia kesi ya uchaguzi


Bwana Raila Odinga

Mahakama ya Juu Kenya,yatupilia mbali ushahidi mpya wa bwana Odinga katika kesi ya kupinga matokeo ya kiti cha rais.

Mahakama ya juu nchini Kenya imetupilia mbali ombi la bwana Raila Odinga la kuongeza ushahidi mpya katika kesi aliyowasilisha awali, kupinga matokeo ya kiti cha rais ambapo tume huru ya uchaguzi ilimtangaza bwana Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na kufuatiliwa moja kwa moja na umma kupitia vyombo vya habari nchini humo, majaji wa mahakama hiyo ya juu wameamrisha leo Jumanne kuwa ushahidi huo mpya wa kurasa 839 ufutwe kabisa kwenye rekodi za mahakama hiyo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mapema Jumanne mahakama hiyo pia ilitupilia mbali ombi lingine la bwana Odinga akitaka ukaguzi wa kitaalam ufanywe kwa tekinolojia ya kimitambo iliyotumiwa na tume huru ya uchaguzi Kenya I.E.B.C. Mahakama hiyo ya juu, ilisema imefikia uamuzi huo kwa sababu ombi la bwana Odinga lilifika kwenye mahakama hiyo kwa kuchelewa kwa mujibu wa muda unaotambuliwa kisheria.

Majaji wa mahakama hiyo pia walikataa ombi la kundi la wanaharakati wa Katiba Institute kushiriki katika kesi hiyo kama rafiki wa koti. Mahakama ilisema kuwa kundi hilo tayari limeonyesha kubagua mojawapo ya makundi ya upande wa utetezi, hususan Bwana Uhuru Kenyattta na William Ruto.

Kesi ya kuamua ikiwa uchaguzi wa kiti cha rais huko Kenya utarudiwa, au rais mteule Uhuru Kenyatta ataapishwa kuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya, yategemewa kuamuliwa na mahakama hiyo ya juu kabla ya Jumamosi wiki hii.
XS
SM
MD
LG