Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:56

Wakenya wachache wasajiliwa kupiga kura


Vifaa vipya vya kusajili wapiga kura Kenya
Jumanne wiki hii imekuwa siku ya mwisho kwa wakenya kusajiliwa kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao. Lakini mamilioni ya raia nchini humo hawakusajiliwa.

Maafisa wa uchaguzi walisema zoezi hilo lilivurugika kwa kila hatua. Wakenya wengi waliripotiwa kuwa katika harakati za mwisho mwisho Jumanne kusajiliwa kushiriki katika uchaguzi wa mwezi machi mwakani. Lakini wengi walilalamika kuwa walisubiri kwa muda mrefu foleni kupata vitambulisho vya taifa ili kuweza kusajiliwa.

Tume ya binafsi inayosimamia uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC ilisema ilitegemea wakenya milioni 18 watasajiliwa kushiriki uchaguzi huo lakini kufikia Jumapili iliyopita ni wakenya milioni 12 waliokuwa wamesajiliwa. Tume hiyo ya uchaguzi imesma haitaongeza muda wa kusajiliwa.
XS
SM
MD
LG