Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:56

Wakazi wa Tanga nchini Tanzania wazungumzia mauaji ya kinyama.


Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Mkoa wa Tanga nchini Tanzania ulikumbwa na simanzi kubwa baada ya watu wanane kutoka kijiji cha Kibatini kwenye kata ya Amboni kuchinjwa kama wanyama na watu wasiojulikana.

Hali hii ilizusha taharuki kote katika mkoa huo na serikali ya Tanzania imeapa kufanya kila juhudi za kuwapata wale waliotenda vitendo hivyo viovu.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na Mariam Shedafa mwandishi wa habari mkoani Tanga ambaye alikwenda kwenye kijiji hicho kupata taarifa zaidi za tukio hilo na alielezea kwamba kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba watu hao ambao ni wauaji walikuwa wamevaa nguo za kawaida na walikuwa wakizungumza lugha fasaha ya Kiswahili.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:08 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG