Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 10:59

Wakazi wa meneo ya yaliyo chini ya M23 wasema hakuna dalili za usalama


Kujiondoa kwenye mapambano kuliko tangazwa siku 10 zilizopita na waasi wa M23 kutoka mji wa kimkakati wa Kibumba mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hakuna mafanikio.

Hayo yamesemwa na wenyeji wa eneo hilo Jumatatu kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Kundi la M23 limeteka maeneo mengi katika eneo la DRC, jimbo la Kivu Kaskazini katika miezi ya karibuni.

Chini ya shinikizo kali la kimataifa la kusitisha mapigano, waasi waliurejesha mji wa Kibumba kwa jeshi la kikanda Desemba 23, wakiita hatua hiyo ishara ya nia njema kwa ajili ya amani.

Jeshi la Kongo hata hivyo liliyataja makabidhiano ya Kibumba kuwa udanganyifu.

Mkazi mmoja, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu za kiusalama, aliiambia AFP kuwa katika vijiji vyote vya Kibumba na Buhumba M23 bado wako nao, kama ilivyo kwa wanajeshi wa kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki.

XS
SM
MD
LG