Wakaazi wa mji wa Hamburg nchini Ujerumani wamepewa onyo kwamba sumu kutokana na moto uliozuka kwenye ghala katika mji wa Rothenburgsort kilomita chache kusini mashariki mwa Hamburg unaelekea kwenye eneo lao.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa licha ya kutojua jinsi moshi huo unavyobeba sumu mamlaka imeamua kuwahamisha wakaazi 140 wa Hamburg huku wakaazi wengine wa Hamburg wamepewa maelekezo ya kuendelea kukaa nyumbani na kuhakikisha milango na madirisha yao yanafungwa.
Moto huo ulizuka mapema Jumapili na kuendelea kuwaka Jumapili mchana licha ya idadi kadhaa ya vikosi vya zima moto kupambana na hali hiyo. Vifaa vilivyokuwemo ndani ya ghala havikuelezea uhalisia wake mara moja.