Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:12

Wajumbe wakutana Ujerumani kufufua majadiliano kwa ajili ya mabadilko ya hali ya hewa


Viwanda vikitoa moshi Indonesia.Picha ya maktaba

Washauri kutoka karibu mataifa 200 wanakutana Jumatatu, mjini Bonn Ujerumani ili kujaribu kufufua tena juhudi za kukabiliana na kuongezeka joto duniani, wakati vita vya Russia nchini Ukraine vikigubika kitisho kinachotokana na uchafuzi wa hewa na mazingira.

Mkutano wa Jumatatu unatayarisha njia kuelekea duru mpya ya mazungumzo ya Umoja wa Mataifa yatakayofanyika Misri baadaye mwakani.

Kikao hicho pia ni mtihani kuona dhamira ya mataifa katika kukabiliana na matatizo yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, mizozo ya kisiasa ya kikanda. umwagikaji wa damu Ukraine pamoja na kupanda kwa bei za vyakula ulimwenguni.

Wakati akiomba ushirikiano wa kimataifa, mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa anayeondoka Patricia Espinosa amewambia wajumbe kwamba, "siyo vyema kusema kwamba sote tunapitia nyakati ngumu.

" Ni lazima tuelewe kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaendelea kutokea kwa kasi kubwa, na tunahitaji kuongeza kasi ya mashauriano." amesema Espinosa.

XS
SM
MD
LG