Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 12:15

Wajerumani waendelea kusherekea ushindi wa Kombe la Dunia


Mjerumani Mario Goetze akipachika goli pekee la ushindi kumpita kipa wa Argentina Sergio Romero wakati wa muda ziada katika uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro, July 13, 2014.

Wajerumani waamka na kuendelea na sherehe za ushindi wa Kombe la Dunia, huku ukurasa wa kwanza wa magazeti mengi ya nchi hiyo, yakiwa yamepakwa rangi ya bendera ya nchi hiyo, nyeusi-nyekundu- dhahabu, picha ya shuja wao Goetze iikienea kote na vichwa vya maneno vinavosema "Weltmeister" -Mabigwa wa Dunia.

Mario Goetze akibusu Kombe la Dunia huko Maracana Rio de Janeiro ,July 13, 2014.
Mario Goetze akibusu Kombe la Dunia huko Maracana Rio de Janeiro ,July 13, 2014.

Mario Goetze ndiye shujaa wa timu aliyeipatia nchi yake ushindi katika dakika ya 113, pale alipotuliza mpira kwenye gamba la kifua chake kutokana na pasi kutoka Andre Schuerrle na kuupachika wavuni na kumwacha hoi kipa wa Argentina, Sergio Romero.

Ushindi huo wa bao moja kwa bila katika uwanja wa Maracana unaipatia Ujerumani kombe la Dunia kwa mara ya nne, ikiwa ni mara ya kwanza tangu nchi hiyo kuungana tena miaka 24 iliyopita. Na ni nchi ya kwanza ya ulaya kunyakua ushindi huo mkuu katika mabara ya Amerika.

Timu ya Argentina iliweza pia kuonesha ustadi wao mnamo dakika zote 120 ikijaribu sana kusawazisha baada ya kupachikwa bao hilo pekee.

Bastian Schweinsteiger akibeba juu Kombe la Dunia akiwa na wenzake
Bastian Schweinsteiger akibeba juu Kombe la Dunia akiwa na wenzake

Baada ya sherehe za kusisimua za kutoa Kombe la ushindi na mchezaji nyota wa Argentina Lionel Messy kupokea kombe la mchezaji bora, timu ilirudi hotelini ikiwa na huzuni, lakini kupokelewa kwa shangwe na mashabiki.

Lakini mjini Buenos Aires hali haikua nzuru polisi wa kupambana na ghasia walipambana na vijana kwenye uwanja wa makumbusho wa Obelisk ambako maaelfu na malefu ya mashabiki walikusanyika wakisubiri kusherekea ushindi lakini mambo hayakwenda upande wao.

Kinyume na huko Ujerumani mashabiki hawakulala kukiwepo na sherehe kila pembe ya nchi hadi alfajiri ya Jumatatuna katika mji wa Frankfurt bila ya kutazamiwa magari yalianza kukusanyika na kuuzunguka mji kamili kwa kufuatana kwa furaha.

Michuano ikiwa imemalizika jambo la kukumbukwa katika finali ya 2014 ni kwamba kumekuwepo na rekodi chungu nzima kuanzia idadi ya watazamaji kwenye televisheni hadi mawasiliano na majadiliano kwenye mitandao ya kijami magoli 170, iliyopachikwa na hata Rais barack Obama wa Marekani akiipongeza timu ya Marekani kwenye tweeter akiwa anasafiri ndani ya ndege yake ya Airforce One pale ilipofanikiwa kuingia katika duru ya pili.

XS
SM
MD
LG