Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:33

Waislamu Kenya walaani msako wa kiholela


Polisi wafanya msako mtaa wa Eastleigh Nairobi April 5, 2014
Polisi wafanya msako mtaa wa Eastleigh Nairobi April 5, 2014
Baadhi ya viongozi wa jamii ya Wasomali Kenya na viongozi wa Kislamu wamelaani msako mkubwa unaofanya na polisi na kikosi maalum cha kupambana na ghasia mjini Nairobi kufuatia mashambulio na mauwaji ya hivi karibuni huko Kenya.

Viongozi hao wameituhumu serikali kwa kuwalenga Waislamu na hasa Wasomali walipofanya msakao mkubwa wa nyumba moja hadi nyingine katika mtaa wa Eastleigh mwishoni mwa wiki na kuwakamata karibu watu 500.

Mwishoni mwa wiki katika msako mkubwa ulowahusisha karibu polisi elfu sita na wale wa kikosi maalum cha kupambana na ghasia ulifanyika ili kuwasaka mahalifu kufuatia miripuko mitatu ya bomu mjini Nairobi wiki ilyopita.

Mkuu wa wabunge waliowengi Aden Duale mwenye asili ya Kisomali alikua afisa wa kwanza kutishia siku ya Ijuma kwamba atajiondoa kutoka mungano unaotawala wa Jubilee, kutokana na kile alichokieleza ni "kukamatwa kiholewa wakazi wa jamii yake."

Siku ya Jumapili viongozi wa jamii ya Kislamu na Wasomali, walikutana Nairobi na wamelaani kitendo cha polisi kuwakamata na kuwabughudhi watu wakati wa msako wa mtaa wa Eastlegh.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mbunge wa Mvita, Mombasa, Abdulswamad Sharif Nassir anasema, msako huo unaowalenga jamii fulani ya watu ni makosa na inazidisha chuki miongoni mwa wakazi.
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Naibu Spika wa zamani wa bunge la Kenya Farah Maalim, kwa upande wake alisema Jumapili, kwamba polisi wamewaibia raia na kuwabughudhi na kuwakamata wanawake na watu wasohusika na ugaidi.

Mwambi Mwasaru, Mkurugenzi wa kundi la kutetea haki za waislamu Mombasa, Muhuri, anasema polisi wanakiuka haki za binadam na sheria za nchi wanapofanya msako jumla na kwa njia ya kiholela.

Bw Mwasaru anasema makundi ya kutetea haki za binadam yanaitaka serikali itafute mbinu nyingine kuwasaka magaidi na wala si raia wasio na hatia.

Lakini inavyonekana hadi hivi sasa wakuu wa usalama wanatetea mbinu wanaotumia kwani kamishna wa polisi wa County ya Nairobi, Njoroge Ndirangu anasema hawajalenga Eastleigh pekee, bali ni msako uloanza mwezi Februari na utafanyika Nairobi nzima.

Kutokana na msimamo huo Mkurugenzi wa Muhuri anasema watalazimika kufikisha mashtaka mahakamani. Mbunge Sharif Nasser kwa upande wake anasema inabidi kuwepo na mazungumzo kati ya pande zote zinazohusika ili kukabiliana na tatizo jumla la usalama.
XS
SM
MD
LG