Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 10:36

Wahusika wakuu Syria wameanza kujipanga wakati vikosi vya US vikiondoka


Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis

Kasi ya harakati za wanajeshi na mawasiliano ya kidiplomasia yaliongezeka Jumatatu siku ambayo Pentagon imethibitisha kuwa waziri wa ulinzi anayeondoka Jim Mattis ameamuru wanajeshi wa Marekani kuanza kuondoka Syria bila ya kufafanua

Wahusika wakuu ndani na kuzunguka Syria wameanza kuyaweka sawa majeshi yao wakati majadiliano yanaendelea jinsi ya kusonga mbele mara majeshi ya Marekani yakapoondoka nchini humo na mapambano dhidi ya mabaki ya kundi la kigaidi la Islamic State ambalo limejitangazia ukhalifa.

Kasi ya harakati za wanajeshi pamoja na mawasiliano ya kidiplomasia, yaliongezeka Jumatatu siku ambayo Pentagon imethibitisha kuwa waziri wa ulinzi anayeondoka madarakani Jim Mattis ameamuru wanajeshi wa Marekani kuanza kuondoka Syria bila ya kufafanua.

Amri ya kiutendaji kwa Syria imetiwa saini afisa wa wizara ya ulinzi ya Marekani ameithibitisha kwa Sauti ya Amerika-VOA na kuongezea "sitaweza kutoa maelezo zaidi ya operesheni kwa wakati huu".

Rais wa Marekani, Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump

Rais Donald Trump alituma ujumbe wa Twitter siku ya Jumapili kwamba yeye na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan walizungumza kwa simu na kwamba kuondoka kwa Marekani kutakuwa kwa kasi ya pole pole na kwa uratibu wa hali ya juu. Msemaji wa Erdogan alisema Jumatatu kuwa maafisa wa ulinzi wa Uturuki watakutana na wenzao wa Marekani wiki hii.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG