Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 18:10

Wahamiaji wawili wafariki baada ya kugongwa na treni nchini Serbia


Wahamiaji na wakimbizi wakusanyika kwenye mpaka kati ya Serbia na Hungary, Februari 6, 2020.
Wahamiaji na wakimbizi wakusanyika kwenye mpaka kati ya Serbia na Hungary, Februari 6, 2020.

Wahamiaji wawili wamefariki baada ya kugongwa na treni kusini mashariki mwa Serbia, polisi wamesema leo Ijumaa, ikiwa ajali mbaya ya hivi karibuni inayohusisha watu wanaosafiri kupitia nchi hiyo ya Balkan.

Ajali hiyo ilitokea wakati kundi la wahamiaji likitembea kwenye njia za reli Alhamisi usiku karibu na mji wa Pirot, karibu na mpaka wa Bulgaria, msemaji wa polisi wa mji huo ameiambia AFP.

“Kulikuwa giza na treni ya mizigo ikawagonga, watu wawili walifariki kutokana na majeraha,” amesema msemaji huyo wa polisi kwa sharti la kutotajwa jina.

Msemaji huyo wa polisi ameongeza kuwa polisi walikuwa wakifanya kazi kubaini utambulisho na uraia wa waathirika, akisema wanaamini walikuwa miongoni mwa kundi kubwa la wahamiaji.

Serbia iko kwenye njia inayoitwa Balkan inayotumiwa na wahamiaji kuelekea Ulaya magharibi, huku wakikimbia vita na umaskini huko Mashariki ya kati, Asia na Afrika.

XS
SM
MD
LG