“Idadi ya waathirika wa ajali ya boti imefikia 73,” waziri wa afya Hassan al-Ghabash amesema katika taarifa, akiongeza kuwa manusura 20 walikuwa wakitibiwa hospitalini katika bandari ya Syria ya Tartus.
Lebanon ambayo tangu mwaka wa 2019 imekumbwa na mzozo wa kifedha uliotajwa na Benki ya dunia kuwa mbaya zaidi katika nyakati za sasa, imekuwa mahali pa kuanzisha uhamishaji haramu, huku raia wake wakiambatana na wakimbizi wa Syria na Palestina wakilalamika kuitoroka nchi.
Waziri wa uchukuzi Ali Hamie amesema zaidi ya watu 100, wengi wao wakiwa raia wa Lebanon na Syria, walikuwa ndani ya boti hiyo ndogo ambayo ilizama Alhamisi katika bahari ya Meditearania karibu na mji wa Syria wa Tartus.
Maafisa wa Syria wamesema takriban abiriya 150 walikuwa ndani ya boti hiyo.