Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:30

Wahamiaji 61 wakiwemo watoto 9 wameokolewa nje ya visiwa vya Canary


Wahamiaji hao, wanawake 31, wanaume 21 na watoto tisa walihamishiwa katika bandari ya Arguineguin huko Gran Canaria ambako walisaidiwa na huduma za dharura.

Idadi za karibuni zilizochapishwa zinaonyesha kuwa wahamiaji 6,359 wamewasili katika visiwa vya canary hadi April 15 ikilinganishwa na 3,980 muda kama huo mwaka jana .

Ufukwe wa visiwa vya Canary Afrika Magharibi vimekuwa kituo kikuu kwa Spain kwa wahamiaji wanaojaribu kufika Ulaya.

Mwaka 2021 ulikuwa wenye harakati nyingi kwa aina hiyo ya kuvuka katika muongo uliopita, kwa mujibu wa data za wizara ya mambo ya ndani.

Jumla ya wahamiaji 22,316 waliwasili katika visiwa hivyo bila mpangilio mwaka 2021 ukiongezea wahamiaji 23,271 waliowasili mwaka uliopita.

Kundi la kutetea haki -Walking Borders, limesema zaidi ya wahamiaji 4,400 wakiwemo angalau watoto 205 walipotea baharini wakijaribu kufika Spain mwaka 2021, zaidi ya mara mbili ya idadi ya mwaka 2020 na wengine zaidi tangu kundi hilo lianze kuhesabu mwaka 2018.

XS
SM
MD
LG