Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 14:37

Wagonjwa na wafanyakazi wanaondoka katika hospitali ya Shifa huko Gaza

Hali ilivyo katika hospitali ya Shifa huko Gaza City. Nov. 10, 2023
Hali ilivyo katika hospitali ya Shifa huko Gaza City. Nov. 10, 2023

Wagonjwa mahututi ambao hawawezi kutembea wamebaki nyuma pamoja na wafanyakazi wachache. Jeshi la Ulinzi la Israel limekanusha kwamba liliamuru watu waondoke  katika hospitali ya Shifa, ambayo ni kituo kikubwa sana cha matibabu huko Gaza.

Wagonjwa, wafanyakazi na watu wasiokuwa na makazi wanaondoka katika hospitali ya Shifa mjini Gaza leo Jumamosi huku kukiwa na ripoti zinazokinzana kwamba Israel imekipa kituo hicho saa moja kuondoka.

Wagonjwa mahututi ambao hawawezi kutembea wamebaki nyuma pamoja na wafanyakazi wachache. Jeshi la Ulinzi la Israel limekanusha kwamba liliamuru watu waondoke katika hospitali ya Shifa, ambayo ni kituo kikubwa sana cha matibabu huko Gaza.

“Hakuna wakati wowote IDF iliamuru kuhamishwa kwa wagonjwa au timu za matibabu, kiukweli ilipendekeza kwamba ombi lolote la uhamishaji wowote wa kimatibabu litashughulikiwa na IDF”, kundi la kijeshi lilisema katika taarifa ya Jumamosi.

IDF ilisema ilizungumza na mkurugenzi wa hospitali hiyo kuhusu kutoa njia salama kwa watu wanaotaka kuondoka hospitalini.

Forum

XS
SM
MD
LG