Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 14, 2024 Local time: 02:33

Wagombea urais sita nchini DRC waomba hatua zichukuliwe kuzuia wizi wa kura katika uchaguzi ujao


Martin Fayulu, mmoja wa wagombea urais nchini DRC.
Martin Fayulu, mmoja wa wagombea urais nchini DRC.

Wagombea urais sita huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwemo wapinzani wakuu wa Rais Felix Tshisekedi Jumanne wameomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuzuia wizi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika taarifa ya pamoja, wagombea hao wameahidi kushirikiana ili kuzuia uchakachuaji wowote wa matokeo na kuitaka tume ya uchaguzi kuchukua hatua kadhaa, ikiwemo kuchapisha orodha ya wapiga kura na ramani ya vituo vya kupigia kura.

Kumekuwa na hali ya mvutano kabla ya uchaguzi wa tarehe 20 Desemba. Washirika wa kimataifa na makundi ya haki za binadamu yamezishtumu mamlaka kukandamiza wapinzani na uhuru wa kujieleza, madai yaliyokanushwa na serikali.

Wagombea wote wa upinzani wameelezea wasiwasi wao juu ya uwezekano wa wizi wa kura na ukosefu wa uwazi.

“Baada ya utata mwingi na ukosefu wa umakini ambao uligubika shughuli zote za kabla ya uchaguzi, ni muhimu siku chache kabla ya kampeni ya uchaguzi, hatua za haraka zichukuliwe kuokoa mchakato wa uchaguzi,” taarifa yao imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG