Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2020 Local time: 06:08

Amnesty yaitaka Serikali ya Gambia kuwaachia wafungwa wa kisiasa


Watu waandamani mjini Dakar April 22, 2016, dhidi ya shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu nchini Gambia.

Afisa wa Amnesty International anasema wanachama wa upinzani nchini Gambia waliokamatwa mwezi uliopita na serikali ya Rais Yahya Jammeh ni wafungwa wa kisiasa na waachiwe kwa sababu walikuwa wakitoa maoni yao kisiasa kama haki yao inayoelezwa kwenye katiba ya Gambia.

Hii imetokea baada ya maafisa wa Gambia mwishoni mwa juma kuwafungulia mashtaka watu 38 waliokamatwa mwezi uliopita ikiwa ni pamoja na mpinzani mkuu Ousanie Darboe wa chama cha UDP huku kukiwa na njama za kufanya makosa.

Walikamatwa awali na kushitakiwa kwa kukutana kinyume cha sheria na kuchochea ghasia baada ya maandaano wakitaka mabadiliko ya kisiasa na huku wakilaani mauaji ya afisa wa UDP Solo Sandeng aliyekuwa kizuizini.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG